Pages

Saturday, 10 November 2018

IKUNGI SEMINA YA UJASI

                   HODI  MKOA WA SINGIDA WILAYA YA IKUNGI - MWARECO

Mkurugenzi wa Mwambo Realistic Company (MWARECO) akitua wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida tayari kwa kuendesha semina ya Ujasiriamali katika harakati za Tanzania ya viwanda inawezekana.


UJASIRIAMALI

Ujasirimali ni hali ya mtu kuthubutu kufanya au kuanzisha shughuli/kazi yoyote ile kwa lengo la kujiongezea kipato chake, ili mradi tu shughuli hiyo iwe halali.

Hapa akina mama sehemu fulani katika kijiji cha Igima kata ya Igima, Tarafa ya Mngeta, Wilaya ya Kilombero wakiwa wanafurahia kazi ya mikono yao baada ya mafunzo ya ujasiriamali hasa kuhusu kujitengenezea bidhaa wenyewe na kujiongezea kipato binafsi. Mafunzo ambayo yametolewa na kampuni ya Mwambo Realistic chini ya Mkurugenzi wake mwl. Lughano K. Mwambogehela.

Utengenezaji wa batiki pamoja na bidhaa zingine za kiwandani kama vile; sabuni ya maji, dawa za usafi, sabuni za mche, shampoo nk. Pia walijifunza namna ya kutengeneza na kusindika vyakula na vinywaji mbalimbali kama; juice ya matunda, karanga za mayai, keki na vtafunwa mbalimbali.





 Baada ya kuona kazi ya mikono yao, ndiposa walipoamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa na kwa kujiamini kabisa.  waliishia kufurahi na kupeana kongole wao kwa wao.


Wednesday, 7 February 2018

ELIMU YA UJASIRIAMALI
Ni ukweli usiopingika kwamba, kwa sasa watu wengi wametambua kuwa ujasiriamali ndiyo suruhisho pekee la ugumu wa maisha yetu ya kila siku. Hivyo ni muhimu sana kila mmoja wetu kujituma ili aweze kujipatia na kujiongezea kipato chake na cha taifa kwa ujumla, hii itasaidia sana kuendana na kasi ya Tanzania ya viwanda.

Hivyo basi Mwambo Realistic Company (MWARECO) ni wauzaji na wasambazaji wa malighafi zitumikazo kutengenezea sabuni za aina zote, dawa za usafi, mishumaa, mafuta ya mgando na lotion, maji ya betri, chaki na aina mbalimbali za mabatiki. Pamoja na haya yote pia kampuni inatoa elimu ya ujasiriamali bure katika ukurasa huu, gharama yako kubwa ni kutembelea ukurasa huu tu ili kujipatia Elimu bila malipo. Na ukihitaji kupata malighafi popote ulipo utapafikishiwa bila matatizo yoyote.

Anza kwa kufahamu haya yafuatayo



SABUNI YA MCHE
MALIGHAFI
·         Caustic soda.
Mafuta; mawese, mbosa, nyonyo, alizeti nk
·         Maji (H2O).
·         Glycerine: (husaidia mikono isikauke na kuchubuka)
·         Perfume: (lemon ni nzuri kwa kufulia)
·         Chumvi: (huifanya sabuni isiishe haraka na kuifanya iwe nzito)
·         Sodium silicate: (kuweka ubora wa sabuni na muunganiko wa malighafi).




Thursday, 18 January 2018

Friday, 17 February 2017

#USAFI NA MWARECO

#Usafi.
Kwa wakazi wa Morogoro  inawahusu sana.
Mwambo Realistic Company (MWARECO) Kampuni ambayo kwa sasa inashughulika na masuala ya usafi
Tupotayari kukufanyia usafi wa nyumbani kwako, ofisi yako, mazingira ya nyumba na maeneo mbalimbali ya makazi yako kwa gharama nafuu sana.
Kuna kazi za kufanywa kwa mkataba na zisizo za mkataba yaani za kulipwa mara baada ya kukamilisha kazi husika.
Kwa mawasiliano ya haraka
0787032054
0658032054
mwareco@yahoo.com
waweza tembelea blog yetu; Mwambo.com
tweeter. @lmwamboghela.com

KARIBUNI SANA.

Monday, 23 January 2017

Waste product management.

Waste product management is so important everywhere  in our societies.  If the societies fail to manage waste materials they are at higher risk.  So our task is to make sure that every corner of our environment is well cleaned.   Therefore Mwambo Realistic Company is there for housing/building  as well as environmental cleanliness  in general.  We normally offer these services with very cheap cost every where where you are.  
If that is the case do not hesitate to communicate with us so that you can enjoy our services peacefully.
Mob; 0787032054      email; mwareco@yahoo.com  
   


                                                 Maeneo ya Boma road Manispaa ya  Morogoro
"HAPA KAZI TU - 2017"

Mwambo Realistic Company (MWARECO)

Habari njema kwa wote.
Mwambo Realistic Company  (MWARECO) ni kampuni mpya inayojishughulisha na masuala au mambo yasiyopungua 9. Kati ya hayo mojawapo ni suala la usafi wa nyumba/majengo na mazingira kwa ujumla.
Kampuni hii imeanza kutekeleza majukumu yake katika mkoa wa Morogoro hasa maeneo ya Manispaa ya mkoa huu husika.  Kampuni ina rasilimali watu wasichana na wavulana ambao jumla yao ni 25.  Kampuni pia inaona kunahaja ya kuendelea na shughuli zingine za kiuchumi ili kupanua wigo wa ajira kwa vijana ambao hawakubahatika kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Kwa hivi sasa kampuni inamkakati wa kuanzisha shughuli ya kusindika bidhaa ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa matunda ambayo hupatikana kwa msimu tu, lakini pia utunzaji wa mboga za majani kwa minajili ya kuzitumia baadaye zikiwa katika hali yake ya kawaida kabisa.
Hivyo kampuni inatoa wito kwa vijana kukaa mkao wa kula mara zitangazwapo zitumike ipasavyo kabisa.

Kama una swali, ushauri na maoni yoyote unakaribishwa.  kwa mawasiliano yafuatayo;
Simu ya mkononi:  0787032054 au 0658032054 au 0767032054.
Barua pepe:   mwareco@yahoo.com
Blog: Mwambo.com




By  Lughano Mwamboghela
         Mkurugenzi - MWARECO

Thursday, 24 November 2016

Changamoto ya mikopo tatizo ni hili hapa. SOMA



                                              JE HII NI KWELI? 
Kwa serikali ya awamu ya tano?

Katika serikali hii ya awamu ya tano ni takribani mwaka mmoja sasa umeshakatika.
Ni ukweli usiopingika kuwa maisha ya watanzania walio wengi bado ni magumu na ni kama yanazidi kwa ugumu. Kwa mtazamo wa harakaharaka unaweza dhani kuwa kila siku hela inazamia hazina kuu, maana kama leo umepata shilingi 5,000 kesho utapata  3,000 au 4,000 na siku inayofuata unaweza pata chini ya hivyo viwango au ukaanza tena na 5,000 ileile.
Serikali ya awamu ya tano ilipokuwa kwenye kampeni ya uchaguzi ilitangaza kuwasaidia walalahoi yaani watu wa hali ya chini wakiwemo mamantilie, bodaboda na wajasiria mali wadogo wadogo.
Cha ajabu na kushangaza ni kwamba mambo yamekuwa ni kinyume chake kabisa. Kwani watanzania wa kipato cha chini ndo wanafanyishwa kuona ugumu wa maisha tofauti ilivyokawaida. Hakuna pesa kabisa hali ikifahamika kuwa pesa ndiyo kila kitu katika maisha ya mwanadamu.
Akina mama wa familiya mbalimbali ndiyo hasa wanaoumia kwani imezoeleka kwamba wao ndiyo watunzaji wa familiya katika kaya zilizo nyingi. Hao hao akina mama ndiyo kwa sasa hawapatiwi fulsa za mikopo kwenye taasisi zinazokopesha kwani hazioni uwezekano wa marejesho kwa mama huyo akipatiwa mkopo huo, na ukweli ndiyo huo. Na kama wanapatiwa basi kwa riba ya juu na wao wanalazimika kuchukua kwa vile hawana jinsi au namna nyingine.
Wale ambao walikopa kabla ya mabadiliko haya, wengine wanakimbia kaya zao na wengine kuishia kifungoni  na wapo ambao wanajificha kwa kukaa ndani tu kwa kuogopa kukamatwa kupoteza hali ya utu waliokuwa nao awali.

Inasemekana kwamba “wanaoona hela hakuna ni wale waliozoea kupiga dili  je ni kweli?
Kwa mtazamo wangu naweza kusema kuwa usemi huu unaukweli kwa asilimia kidogo sana kwa sababu;      
Wanaoteseka na kuona ugumu wa maisha si wale ambao wamepunguziwa marupurupu na mishahara kuwa midogo, bali ni watanzania waliomasikini. JE HAWA NAO WALIKUWA WANAPIGA MADILI WAPI?
Akina mamantilie, wakulima, waendesha bodaboda, wajasiriamali wadogo na makundi maalum wanamadili gani ya kuwanufaisha? Na ndiyo walio wengi.
Waliokuwa na mishahara ya milioni nyingi wakapunguziwa hadi kubakia milioni chache na wengine wenye mishahara yao wataona kuna mabadiliko kidogo ya hali walioizoea lakini siyo kuona ugumu wa maisha kama wanaouona masikini wasio na kipato cha uhakika.
Kundi kubwa la wasomi waliotoka katika kaya masikini hawana ajira. Tokeo lake ni kwamba wengi wanatumia akili zao kufanya wizi ulioenda shule hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii, bado haohao walalahoi ndiyo wanaibiwa kwa kutojua kwao au kutaka hela/mafanikio ya haraka.

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba; wanapoendelea kubana matumizi basi waangalie maisha ya walala hoi wanapataje mahitaji yao muhimu? Aidha watu waajiriwe ili kuruhusu mzunguko wa fedha kwa watu walio wengi kuliko sasa kuna kundi kubwa ambalo ni tegemezi.
Yaani inatia huruma sana ukiwaona akina mama mitaani wanavyohangaika namna ya kurejesha mikopo yao.   
                                                 MUNGU IBARIKI TANZANIA. 
                                 BARIKI SERIKALI YETU NA UTENDAJI WAKE.