JE HII NI KWELI?
Kwa serikali ya awamu ya tano?
Katika serikali hii ya awamu ya tano ni takribani mwaka
mmoja sasa umeshakatika.
Ni ukweli usiopingika kuwa maisha ya watanzania walio wengi
bado ni magumu na ni kama yanazidi kwa ugumu. Kwa mtazamo wa harakaharaka unaweza
dhani kuwa kila siku hela inazamia hazina kuu, maana kama leo umepata shilingi
5,000 kesho utapata 3,000 au 4,000 na
siku inayofuata unaweza pata chini ya hivyo viwango au ukaanza tena na 5,000
ileile.
Serikali ya awamu ya tano ilipokuwa kwenye kampeni ya
uchaguzi ilitangaza kuwasaidia walalahoi yaani watu wa hali ya chini wakiwemo
mamantilie, bodaboda na wajasiria mali wadogo wadogo.
Cha ajabu na kushangaza ni kwamba mambo yamekuwa ni kinyume
chake kabisa. Kwani watanzania wa kipato cha chini ndo wanafanyishwa kuona
ugumu wa maisha tofauti ilivyokawaida. Hakuna pesa kabisa hali ikifahamika kuwa
pesa ndiyo kila kitu katika maisha ya mwanadamu.
Akina mama wa familiya mbalimbali ndiyo hasa wanaoumia kwani
imezoeleka kwamba wao ndiyo watunzaji wa familiya katika kaya zilizo nyingi.
Hao hao akina mama ndiyo kwa sasa hawapatiwi fulsa za mikopo kwenye taasisi
zinazokopesha kwani hazioni uwezekano wa marejesho kwa mama huyo akipatiwa
mkopo huo, na ukweli ndiyo huo. Na kama wanapatiwa basi kwa riba ya juu na wao
wanalazimika kuchukua kwa vile hawana jinsi au namna nyingine.
Wale ambao walikopa kabla ya mabadiliko haya, wengine
wanakimbia kaya zao na wengine kuishia kifungoni na wapo ambao wanajificha kwa kukaa ndani tu
kwa kuogopa kukamatwa kupoteza hali ya utu waliokuwa nao awali.
Inasemekana kwamba “wanaoona
hela hakuna ni wale waliozoea kupiga dili”
je ni kweli?
Kwa mtazamo wangu naweza kusema kuwa usemi huu unaukweli kwa
asilimia kidogo sana kwa sababu;
Wanaoteseka na kuona ugumu wa maisha si wale ambao
wamepunguziwa marupurupu na mishahara kuwa midogo, bali ni watanzania
waliomasikini. JE HAWA NAO WALIKUWA WANAPIGA MADILI WAPI?
Akina mamantilie, wakulima, waendesha bodaboda,
wajasiriamali wadogo na makundi maalum wanamadili gani ya kuwanufaisha? Na
ndiyo walio wengi.
Waliokuwa na mishahara ya milioni nyingi wakapunguziwa hadi
kubakia milioni chache na wengine wenye mishahara yao wataona kuna mabadiliko
kidogo ya hali walioizoea lakini siyo kuona ugumu wa maisha kama wanaouona
masikini wasio na kipato cha uhakika.
Kundi kubwa la wasomi waliotoka katika kaya masikini hawana
ajira. Tokeo lake ni kwamba wengi wanatumia akili zao kufanya wizi ulioenda
shule hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii, bado haohao walalahoi ndiyo
wanaibiwa kwa kutojua kwao au kutaka hela/mafanikio ya haraka.
Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba; wanapoendelea kubana
matumizi basi waangalie maisha ya walala hoi wanapataje mahitaji yao muhimu?
Aidha watu waajiriwe ili kuruhusu mzunguko wa fedha kwa watu walio wengi kuliko
sasa kuna kundi kubwa ambalo ni tegemezi.
Yaani inatia huruma sana ukiwaona akina mama mitaani
wanavyohangaika namna ya kurejesha mikopo yao.
MUNGU
IBARIKI TANZANIA.
BARIKI SERIKALI YETU NA UTENDAJI WAKE.
No comments:
Post a Comment