Hapa akina mama sehemu fulani katika kijiji cha Igima kata ya Igima, Tarafa ya Mngeta, Wilaya ya Kilombero wakiwa wanafurahia kazi ya mikono yao baada ya mafunzo ya ujasiriamali hasa kuhusu kujitengenezea bidhaa wenyewe na kujiongezea kipato binafsi. Mafunzo ambayo yametolewa na kampuni ya Mwambo Realistic chini ya Mkurugenzi wake mwl. Lughano K. Mwambogehela.
Utengenezaji wa batiki pamoja na bidhaa zingine za kiwandani kama vile; sabuni ya maji, dawa za usafi, sabuni za mche, shampoo nk. Pia walijifunza namna ya kutengeneza na kusindika vyakula na vinywaji mbalimbali kama; juice ya matunda, karanga za mayai, keki na vtafunwa mbalimbali.
Baada ya kuona kazi ya mikono yao, ndiposa walipoamini kuwa wanaweza kufanya mambo makubwa na kwa kujiamini kabisa. waliishia kufurahi na kupeana kongole wao kwa wao.
No comments:
Post a Comment