Mwambo Realistic Company (MWARECO) ni kampuni mpya inayojishughulisha na masuala au mambo yasiyopungua 9. Kati ya hayo mojawapo ni suala la usafi wa nyumba/majengo na mazingira kwa ujumla.
Kampuni hii imeanza kutekeleza majukumu yake katika mkoa wa Morogoro hasa maeneo ya Manispaa ya mkoa huu husika. Kampuni ina rasilimali watu wasichana na wavulana ambao jumla yao ni 25. Kampuni pia inaona kunahaja ya kuendelea na shughuli zingine za kiuchumi ili kupanua wigo wa ajira kwa vijana ambao hawakubahatika kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Kwa hivi sasa kampuni inamkakati wa kuanzisha shughuli ya kusindika bidhaa ili kukabiliana na tatizo la uharibifu wa matunda ambayo hupatikana kwa msimu tu, lakini pia utunzaji wa mboga za majani kwa minajili ya kuzitumia baadaye zikiwa katika hali yake ya kawaida kabisa.
Hivyo kampuni inatoa wito kwa vijana kukaa mkao wa kula mara zitangazwapo zitumike ipasavyo kabisa.
Kama una swali, ushauri na maoni yoyote unakaribishwa. kwa mawasiliano yafuatayo;
Simu ya mkononi: 0787032054 au 0658032054 au 0767032054.
Barua pepe: mwareco@yahoo.com
Blog: Mwambo.com
By Lughano Mwamboghela
Mkurugenzi - MWARECO
No comments:
Post a Comment