Pages

Saturday, 25 June 2016

ATHARI ZA MADEREVA WAZEMBE KATIKA TAIFA.

Madereva wazembe ni wale ambao wanadhaniewa kutokuwa makini na kazi yao eidha kwa kuwa na mtazamo finyu unaoambatana na weledi katika kazi zao. Kwani ni ukweli usiofichika kuwa dereva mzembe awapo katika stering ya chombo chake hujiona kuwa yeye ndo yeye wengine wote waliomo katika chombo anachokiongoza wanaonekana si kitu. Dereva wa namna hiyo hafai kufanya kazi hiyo. Dereva mwenye hofu na watu waliomo katika chombo anachokiongoza huthamini kwa dhati utu wa watu aliowabeba na anafahamu kuwa abiria na dereva ni watu na wote wanapenda kufikia malengo kuntu katika maisha. Ninaomba kwa moyo wa dhati kabisa kuwaasa madereva kuacha uzembe wa makusudi kwani uzembe husababisha ajali na athari za ajali hizo ni nyingi tena zinatisha, chache kati ya hizo nyingi ni kama ifuatavyo; > Kupoteza nguvu kazi katika taifa; nadhani hii inafahamika sana na iko wazi mno kuwa ajali inapotokea watu wengi wanakufa bila kuchagua watoto, wazee au hata vijana. Hivyo nguvu kazi kubwa inapotea kwa mara moja. > Kundi la watu tegemezi; mara baada ya ajali kutokea, ghafla watu wenye nguvu zao na ambao awali kabla ya ajali kuwakuta walikuwa wanategemewa na taifa, familiya zao na katika jamii kwa ujumla wanajikuta kuwa ni tegemezi na wengine kujikuta wanaanza kuwa ombaomba katika jamii wanamoishi. > Si hayo tu bali pia magonjwa ya kuambukizwa; ajali inapotokea msukosuko mkubwa na tafrani hutokea. Katika tafrani hiyo wengine hupoteza maisha lakini pia wengine hupata majeraha lakini hawakutwi na umauti lakini hupata magonjwa ya kuambukiza kama vile UKIMWI. Hii ni kwa sababu damu ya mtu mmoja huchanganyikana na ya mwingine hivyo kama kuna mwathirika anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuambukiza ugonjwa. > Kuongezeka kwa machokoraa katika jamii; inapotokea baba na mama au walezi wanapopoteza uhai kwa sababu ya uzembe wa dereva mzembe, basi wale wote wanaowategemea hasa watoto wanaanza kuwa ombaomba katika jamii wanamoishi. Zipo athari nyingi sana. Hapa jambo la muhimu sana ni madereva kuuacha uzembe wanapoendesha vyombo vya kubeba abiria. Dereva ACHA UZEMBE kwani athari za uzembe wako ni kubwa katika ujenzi wa Taifa. Jaribu kutumia muda kufikiri hili kwa kina na kisha epuka lawama na laana za wanandugu wanaopotelewa na ndugu zao. Mungu wabariki madereva wawe na moyo wa busara wawapo kazini kwa ustawi wa jamii inayopaswa kukuabudu. CHANGIA MAWAZO YAKO TUOKOE TAIFA LETU. 2016

No comments:

Post a Comment